Mtaala Mpya na Utendaji wa Wanafunzi wa Kiswahili Katika Shule za Upili Mjini Mbarara
DOI:
https://doi.org/10.59472/jodet.v2i1.59Abstract
Utafiti ulikuwa unahusu kutambua mchango wa mtaala mpya katika ufundishaji wa wanafunzi wa Kiswahili wa shule za upili zilizochaguliwa jijini kusini mwa Mbarara na ulilenga kutambua umuhimu wa mtaala mpya katika ufundishaji wa wanafunzi wa Kiswahili katika shule za upili, kuchunguza changamoto zinazokumba wanafunzi na walimu wa Kiswahili katika ufundishaji wa mtaala mpya na kutambua njia zinazotumiwa kutatua changamoto zinazosababishwa na mtaala mpya. Watafiti walituia mbinu ya maelezo, Watafiti walikuwa makini katika kueleza, kufafanua, kuhakiki, kuvumbua, kufanya majaribio, kutafsiri taarifa walizozipata kupitia muundo huu wa utafiti. Sehemu ndogo ya utafiti ilitumia takwimu kama kielelezo na ulifanyika katika shule za upili zilizochaguliwa jijini kusini mwa Mbarara, Utafiti huu ulilenga walimu na wanafunzi wa shule za upili wanoajifunza lugha ya Kiswahili. Katika utafiti huu taarifa mbalimbali zilikusanywa kutoka maktabani na uwandani kwa kutumia mbinu na vifaa mbalimbali vilivyoandaliwa na watafiti. Watafiti walichunguza na kuchanganua data za watafitiwa kulingana na kiwango cha jinsia na umri katika shule za upili.
Utafiti huu ulihitimisha kwamba mtaala mpya wa Kiswahili unahusiana sana na utendaji kitaaluma kwa wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili lakini ili kuiendeleza mtaala mpya ipasavyo ni jukumu la walimu wakuu, walimu, wazazi, wanafunzi, serikali pamoja na kituo kikuu cha mtalaa ni lazima kujiunga pamoja kwa lengo moja na ulipendekeza kwamba Wizara ya elimu iangalie kwamba walimu wamepewa elimu ya ziada kuhusu mabadiliko ya mtaala mpya ili kupata ujuzi na stadi za kufundisha vyema. Walimu wakipewa elimu ya ziada wanapata stadi na hamu ya kwendeleza mtaala mpya jambo linaloletea wanafunzi kufaulu mitihani kwa sababu watakuwa wanapata mwongozo mzuri kutoka walimu, Pengine lazima viongozi wa shule wajaribu huku na kule kuona kwamba wamenunua vitabu vya kiada na vifaa vingine kama miongozo ya walimu inayofasili vitabu vya kiada. Jambo hili huwezesha walimu kufundisha bora wanafunzi na mwishoni wanazuka na utendaji bora kitaaluma.
References
Allright, R. L. (1981). What do we want teaching materials for? ELT Journal, 36 (1), 5-18.
Babusa, H. (2010). Uchanganuzi Linganuzi wa Mielekeo na Umilisi wa Lugha ya Kiswahili wa Wanafunzi Katika Mikoa ya Pwani na Nairobi Nchini Kenya.
Besha, R. M. (1994). Utangulizi wa lugha na isimu. Dar-res-Salaam: Dar-es-Salaam University Press:
Brown, H. D. (2007). Principles of Language Learning and Teaching (5th Ed.). New York: Pearson Education White Plains
Buliba na wenzake (mwaka haujulikani). Misingi ya Nadharia na mbinu za utafiti. Mwanza: Serengeti Educational publishers.
Celce-Murcia, M. (1991). Grammar Pedagogy in Second and Foreign Language Teaching. New York: Newburry House.
Cohen, L. (1980). Research methods in Education (5th edition). London: Rutledge. Falmer.
Enon, C. J. (1995). Educational Research, Statistics and Measurement. Kampala: Makerere University Press.
Haki Elimu, (2011). Je walimu wetu wana sifa za ualimu na hamasa ya kufundisha? Dar-es- Salaam: Haki Elimu.
Downloads
Published
How to Cite
License
Copyright (c) 2024 Murokozi Cranimah
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors retain copyright, and full publishing rights and grant the journal a right of first publication with the work as licensed under the Creative Commons License CC that allows others to share the work with an acknowledgment of the author and initial publication in this journal.